Gor Mahia yakaza kamba kwenye ligi

  • | Citizen TV
    129 views

    Mabingwa watetezi Gor Mahia sasa wako pointi tatu nyuma ya viongozi wa ligi kuu Police FC baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya KCB katika mechi iliyopangwa upya iliyochezwa kwenye uwanja wa Machakos. Mechi hiyo hapo awali ilipangwa kufanyika Jumapili alasiri lakini mvua kubwa huko Machakos ilifanya uwanja kujaa maji na usichezeke. Gor Mahia ilifunga bao la pekee katikati ya kipindi cha kwanza kutoka kwa nahodha austin odhiambo katika dakika ya 32. Wakiwa na mechi moja ya ziada, gor mahia wamezoa pointi 46, pointi mbili nyuma ya tusker fc katika nafasi ya pili na pointi tatu nyuma ya viongozi Police FC.