Hakuna usawa kwenye miundomsingi ya shule za msingi

  • | Citizen TV
    143 views

    Kutokuwa na usawa kwenye miundomsingi ya shule za msingi humu nchini kunazidi kutatiza kiwango cha masomo yanayotolewa haswa katika shule za umma, ikilinganishwa na shule za kibinafsi. Wadau katika sekta ya elimu wanaitaka serikali kuwekeza zaidi kwenye miundomsingi katika shule za umma ili kuhakikisha kuwa wanafunzi nchini wanapata fursa sawa na kuimarisha matokeo katika shule za umma. Na kama anavyoarifu Brenda Wanga, utekelezaji kikamilifu wa mtaala wa CBC unategemea pakubwa kuimarishwa kwa miundomsingi katika shule za umma.