Hatimaye Kaunti ya Nairobi imeondoa uchafu nje ya Stima Plaza

  • | Citizen TV
    478 views

    Hatimaye serikali ya kaunti ya Nairobi imesafisha eneo lililotupwa taka nje ya makao makuu ya kampuni ya Kenya Power, mtaani Ngara Nairobi. Hii ni kufuatia makataa iliyotolewa na mamlaka ya mazingira, NEMA pamoja na Wizara ya Afya. Kaunti ikisema eneo hilo sasa ni salama kwa umma na kwamba mzozo wa madeni baina ya kaunti hiyo na Kenya Power umetatuliwa.