‘Hatusaidiwi na Rwanda,’ asema kiongozi wa M23 Corneille Nangaa

  • | BBC Swahili
    5,824 views
    Kiongozi wa kundi la waasi wenye silaha ambao wanalishikilia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ameiambia BBC kwamba watakwenda hadi mji mkuu Kinshasa, takriban kilomita 1,500, ikiwa watavamiwa na vikosi vya serikali. Corneille Nangaa, ambaye anaongoza muungano unaojumuisha waasi wa M23, amekana kupokea usaidizi wa kijeshi kutoka Rwanda. Pia amesema hana taarifa za ukiukwaji wowote wa haki za binadamu unaofanywa na M23.