Hospitali ya rufaa na mafunzo ya Kilifi inadai Ksh.300m za SHA

  • | Citizen TV
    90 views

    Kamati ya seneti ya uwekezaji wa umma kwenye kaunti, imeelezea hofu ya kusambaratika kwa huduma za afya kwenye hospitali za umma, baada ya kutembelea hospitali kuu ya rufaa na mafunzo ya Kilifi. Kamati hiyo iligundua kuwa hospitali hiyo inadai serikali deni la bima mpya ya matibabu ya SHA, jumla ya shilingi milioni 310. Kamati hiyo ambayo imekua pwani ya imetembelea miradi mbali mbali mjini Mombasa, Kilifi na Malindi. Kulingana na gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro deni hilo la zaidi ya shilingi milioni 300 limesababisha uhaba wa dawa na vifaa vya matibabu hospitalini humo.