- 219 viewsPolisi wa Uganda wamesema Jumapili kuwa idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya ardhi kwenye eneo kubwa la kutupia taka mjini Kampala imefikia 21, wakati timu za uokozi zikiendelea kutafuta manusura na idadi ya miili inayopatikana ikielekea kuongezeka. Kwa mujibu wa shirika la habari, mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha katika wiki za karibuni zilisababisha kuporomoka kwa sehemu ya eneo hilo, ambalo ndilo pekee linalotumika kutupa takataka mjini humo, na kupelekea kufunikwa kwa baadhi ya nyumba zilizokuwa karibu, wakati wenyewe walipokuwa wamelala. Mamlaka za jiji Jumamosi zilisema kuwa watu 8 walikufa, lakini kufikia leo idadi hiyo imeongezeka hadi 21, huku wengine 14 walijeruhiwa. Kati ya waliofariki miili isiyopungua miwili ilikuwa ya watoto. Shirika la Msalaba mwekundu nchini humo limesema kuwa mahema yamewekwa karibu na eneo la tukio, ili kutoa hifadhi kwa watu walioathiriwa. Eneo hilo linalofahamika kama Kiteezi, kwa miongo mingi limekuwa likitupwa taka taka za Kampala, hadi kugeuka na kuwa mlima, huku wakazi waishio karibu wakilalamika kutokana na taka zenye sumu, pamoja na uharibifu wa mazingira. Nchini Ethiopia, takriban watu 115 walikufa 2017 baada ya eneo la taka mjini Addis Ababa kuporomoka, huku wengine 17 wakifa 2018, mjini Maputo, Msumbiji, kwenye tukio sawa na hilo. – Reuters, AP, VOA #uganda #kampala #takataka #dumpo #maporomoko #vifo #polisi #voa #voaswahili
Idadi ya vifo katika eneo la kutupia takataka vyafikia 21
- 27 Nov 2024 - Interior Principal Secretary Raymond Omollo has undescored Kenya’s steadfast commitment to combating terrorism and violent extremism.
- 27 Nov 2024 - The High Court has directed that a case challenging government’s requirement for passengers entering Kenya to declare the International Mobile Equipment Identity (IMEI) numbers be heard on December 18, 2024.
- 27 Nov 2024 - The officer, an Officer Commanding Station (OCS) from Trans Nzoia County, was reportedly demonstrating the weapon's operation to a drinking companion when the firearm discharged, striking the bar attendant in the stomach.
- 27 Nov 2024 - The National Assembly has scoffed at reports claiming that some Members of Parliament (MP) have been misappropriating allowances meant for their drivers and bodyguards.
- 27 Nov 2024 - An 18-year-old Form Four leaver died after he was mauled by a hippopotamus at Kokina beach in West Yimbo location Usigu sub-county within Siaya County last evening.
- 27 Nov 2024 - The clarification comes after a public uproar by Kenyans online.
- 27 Nov 2024 - The decision came after the vetting conducted by Members of Parliament on Friday, November 22.
- 27 Nov 2024 - Officers from the Wajir Township Police Station, who were patrolling the town, arrived quickly and discovered Senior Sergeant Lonzi Joseph, a member of the Department of Defence (DoD) stationed in Wajir, as the victim of the attack.
- 27 Nov 2024 - She is among several other inmates and prison wardens who benefitted from the programme.
- 27 Nov 2024 - Kenyan terms the ceasefire as a vital step towards restoring peace in the Middle East region.