Idadi ya waliofariki wakati wa maandamano umefika watu 26

  • | Citizen TV
    2,291 views

    Idadi ya waandamanaji waliofariki kufuatia maandamano sasa imefikia 26 baada ya watu wawili zaidi kuaga dunia. Kijana wa miaka 22 Kevin Mandaga alifariki mjini Nakuru kufuatia majeraha ya risasi aliyopata kwenye maandamano ya jumanne iliyopita. Katika kaunti ya Bungoma, kijana mwingine wa miaka 17 Daniel Kakai pia amefariki. Idadi hii ikiongezeka huku maandamano zaidi yakipangiwa kuendelea hapo kesho