Idara ya upelelezi yataka maafisa wa kaunti ya Nairobi kuhojiwa kuhusu sakata la taka Stima Plaza

  • | K24 Video
    16 views

    Idara ya upelelezi, sasa imewataka viongozi wa ngazi za juu katika serikali ya kaunti ya Nairobi akiwemo afisa mtendaji katika wizara ya mazingira Geoffrey Mosiria waandikishe taarifa kuhusiana na kumwagwa kwa taka nje ya jengo la Stima Plaza hapa jijini Nairobi. Haya yanajiri huku maafisa wawili wandamizi wa serikali ya kaunti wakisimamishwa kazi na Gavana Johnson Sakaja kuhusiana na suala hilo.