Jamaa agongwa na gari la msafara wa Rais Ruto

  • | Citizen TV
    21,544 views

    Raia mmoja wa ufaransa amefariki baada ya kugongwa na gari ambalo lilikuwa linaendeshwa kwa kasi kwenye msafara wa magari ya Rais William Ruto, katika ziara yake ya maeneo bunge ya Kibra na Lang’ata. Raia huyo ambaye hajatambuliwa jina alifariki papo hapo. Haya yanajiri huku vurugu zikishuhudiwa katika shule ya msingi ya Ayany, maafisa wa polisi wakikabiliana na vijana waliotaka kuingia kwenye uga wa shule hiyo alikokuwa rais.