Skip to main content
Skip to main content

Jamii ya Murule yamuidhinisha Ali Maalim Hassan kuwania ubunge Mandera Mashariki

  • | Citizen TV
    132 views
    Duration: 1:13
    Jamii ya Murule katika kaunti ya Mandera imekubaliana kwa kauli moja kumuunga mkono Ali Maalim Hassan kugombea kiti cha eneo bunge la Mandera Mashariki katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Hii ni baada ya mikutano ya mashauriano na wagombea kiti wengine wa jamii hiyo ili kuepuka mgawanyiko ambao umepelekea jamii hiyo kupoteza kiti hicho katika chaguzi zilizopita. Maalim anatarajiwa kuleta uwiano baina ya jamii zingine katika eneo hilo ambalo limeshuhudia mapigano ya kikabila wakati wa ukame sawa na kuboresha hali ya elimu na ajira kwa vijana.