Je, Israel na Hamas watasitisha vita Gaza? Yote katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    6,078 views
    Huko Mashariki ya Kati, Israel imewaachia huru zaidi ya wafungwa 600 wa Kipalestina kama sehemu ya mwisho ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza. Mabasi yaliyokuwa yamewabeba wapalestina yaliwasili Ramallah katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na walowezi. Hatua hii inajiri baada ya Hamas kutoa miili ya mateka wanne wa Israel waliofariki. Hamas imesema iko tayari kuanza mazungumzo yaliyocheleweshwa kuhusu hatua inayofuata ya usitishaji wa vita Gaza.