- 5,496 viewsDuration: 1:47Je, unahisi maumivu au uchungu unapoenda haja ndogo, au unajikuta kila wakati unahitaji kukojoa? Hizi ni baadhi ya dalili za maambukizi ya njia ya mkojo (UTI). Takribani mmoja kati ya wanawake 2 hupata UTI , huku wanaume wakiwa takriban 20% tu ya visa vyote. Utafiti wa Daktari Katherine Keenan uliofanyika Tanzania, Kenya, na Uganda ulionyesha kuwa maambukizi sugu na yasiyoonyeshwa dalili yapo kwa nusu ya wanawake waliopimwa. @_phillys anatueleza zaidi: