Kalonzo amtaka Rais Ruto kukomesha ukatili kwa raia

  • | Citizen TV
    1,237 views

    Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amekashifu vikali utekaji nyara wa kiholela nchini na kutaja visa hivyo kama ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadam. Katika hotuba yake ya mwisho mwaka huu, kiongozi huyo wa upinzani amedai kuwa wanaotekeleza utakaji nyara ni kundi linalojulikana vizuri na serikali. Kalonzo sasa anamataka rais william ruto kusitisha maovu hayo.