Kamaliza FC waibuka mabingwa wa makala ya nne ya kombe la Mannabay

  • | Citizen TV
    1,587 views

    Kamaliza FC yenye makao yake mjini Kajiado ndio mabingwa wa makala ya nne ya kombe la mannabay baada ya kuwanyuka Purko FCmbili bila kwenye fainali iliyochezwa katika uga wa ildamat mjini Kajiado. Michuano hiyo ambayo pia ilihusisha mchezo ya voliboli huandaliwa kila mwaka katika kaunti za kajiado na Nakuru na wakfu wa Mannabay, inalenga kuwaleta vijana pamoja ili kuwahamasisha kuhusu changamoto mbali mbali zinazowakumba, ikiwemo kuepuka matumizi ya mihadarati, na maadili katika jamii.