Kamati ya elimu yatoa muda wa saa ishirini na nne kwa usimamizi wa chuo kikuu cha Moi

  • | K24 Video
    177 views

    Kamati ya elimu ya bunge la taifa imetoa muda wa saa ishirini na nne kwa usimamizi wa chuo kikuu cha Moi kupata mwafaka na wahadhiri na wafanyikazi wa chuo hicho wanaoshiriki mgomo wa miezi miwili sasa. Wafanyikazi hao wenye ghadhabu walimzoma mno naibu mkuu wa chuo hicho profesa Isaac Kosgei mbele ya mwenyekiti wa kamati hiyo Julius Meli wakitaka mabadiliko ya usimamizi. Haya yanawadia huku viongozi wa muungano wa kitaifa wa wahadhiri ukitangaza kuendelea kwa mgomo wao.