Kampeni ya kumuinua mtoto wa kiume yazinduliwa Baringo

  • | Citizen TV
    104 views

    kampeni maalum ya kumuinua mvulana imezinduliwa katika kaunti ya Baringo ili kurejesha nafasi yake katika jamii. Kampeni hii inalenga kukabiliana na changamoto zinazomkumba mvulana kama vile matumizi ya dawa za kulevya, kujiunga na magenge ya uhalifu, na kushuka kwa hali ya kujiamini. Akizungumza huko Kapkirwok, Baringo Kaskazini, mwanaharakati wa elimu Wycliffe Tobole , wakati umefika wa serikali kumwangazia mvulana katika juhudi za kufanikisha usawa wa kijinsia. wakereketwa hao wamesema kuwa jamii inapaswa kubadili mtazamo na kuanza kumlea mvulana kwa upendo na uangalizi sawa na msichana, ili kujenga kizazi chenye usawa, nidhamu na maadili kwa wote.