Kampuni ya Alef Aeronautics yaonyesha gari la umeme likiruka

  • | VOA Swahili
    4 views
    Kampuni moja ya California, hapa Marekani, imepiga hatua nyingine katika juhudi za kufanikisha lengo lake la kutengeneza na kuuza magari yanayoruka, kwa kutumia teknolojia ya kipekee. Alef Aeronautics, ilionyesha mfano wa gari lake linalotumia nishati ya umeme. Katika hafla iliyohudhuriwa na waandishi habari pekee, gari hilo lilionekana likinyanyuka kutoka ardhini kwa utaratibu, kupaa kwa sekunde kadhaa, na kutua wima. BMJ Muriithi anaarifu zaidi. #california #marekani #gari #nishati #umeme #teknolojia #voa #voaswahili