- 5,107 viewsDuration: 3:12Seneta wa Nandi Samson Cherargei amejipata mashakani kufuatia matamshi yake ya kuunga mkono utekaji nyara wa wanaharakati wa kenya kwenye mataifa jirani. Cherargei aliyezungumza kanisani huko kapsabet siku ya jumapili alipongeza viongozi wa uganda na tanzania kwa kukabiliana na wanaharakati na kusema kenya itamalizia pale walipowachia. Na kama gatete njoroge anavyoarifu, kanisa la KAG alikozungumzia Cherargei limejitenga na matamshi hayo huku seneta huyo akishikilia kuwa hataomba msamaha.