- 4,134 viewsDuration: 53sKinara wa chama cha People's Liberation Party Martha Karua ameMshtumu rais William Ruto kwa kuendeleza siasa za matusi dhidi ya viongozi wa upinzani. Akizungumza mjini Hola kaunti ya Tana river, Karua amemtaka rais kuwatumikia wananchi na kutekeleza aliyowaahidi badala ya kuendeleza matusi. Karua vilevile amejipigia debe kama kiongozi atayebadilisha maisha ya wakenya na kuwarai wakazi kumpa majukumu ya kuliongoza taifa kwenye uchaguzi mkuu ujao