Kaunti ya Busia yaongoza kwa upanzi wa miti ya mianzi

  • | Citizen TV
    177 views

    Wakulima katika kaunti ya Busia na taifa kwa jumla wamehimizwa kuendelea kupanda mianzi kwa wingi kwa lengo la kupunguza uharibifu wa misitu . Kaunti ya Busia ikiwa miongoni mwa kaunti zinazoongoza katika upanzi na utumizi wa mianzi, vijana kutoka kaunti zingine nchini wanazidi kumiminika katika kaunti hiyo ili kujifunza mengi kuhusu mmea huo.