Kaunti ya Kilifi imezindua mafunzo kwa walimu wa shule za upili

  • | Citizen TV
    155 views

    Serikali ya kaunti ya kilifi ikishirikiana na washikadau katika sekta ya uvumbuzi imezindua mpango maalum wa kuwafundisha walimu wa shule za upili kaunti hiyo kwa lengo la kuboresha elimu ya kidigitali. Kulingana na gavana Gideon Mung’aro mpango huu ni mojawapo ya mipango itakayoboresha mafunzo ya kidigitali na kutoa nafasi kwa wanafunzi kaunti hiyo kufaidika na taaluma hiyo muhimu. Aidha washikadau walioshirikiana na serikali ya kaunti ya kilifi wamewekeza dola laki nne.