Kaunti ya Lamu yaweka mikakati ya kuboresha sekta ya uvuvi

  • | Citizen TV
    418 views

    Asilimia zaidi ya 28 ya samaki wanaovuliwa baharini kila siku katika kaunti ya Lamu huharibika na kutupwa kutokana na wavuvi kukosa vifaa vya kuhifadhi samaki. Aidha serikali ya kaunti ya Lamu imeanzisha mikakati ya kuboresha sekta ya uvuvi ili wavuvi wasipate hasara tena.