Kero La Mihadarati: Wanaharakati waomba usaidizi wa serikali

  • | KBC Video
    24 views

    Viongozi wa vijana katika wadi za Mwea na Makima kaunti ya Embu wanatoa wito kwa serikali kuyasaidia mashirika yanayoendeleza vita dhidi ya uraibu wa mihadarati na pombe. Viongozi hao wanasema kampeni za uhamasisho kuhusu madhara ya utumizi wa mihadarati na ubugiaji pombe zinapaswa kuimarishwa miongoni mwa vijana ambao wengi wao wanatekwa na uraibu huo. Mdhamini wa kundi la vijana la Mwema, Nicholas Kasanga amesema kampeni hiyo inaweza kufanikiwa endapo viongozi katika eneo hilo watashirikiana na serikali kufanikisha juhudi za wale wanaopambana na uovu huo. kasanga alisema hayo wakati wa warsha ya kuhamasisha vijana katika Parokia ya Kitololoni ya kanisa Katoliki eneo la Makima.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive