- 1,181 viewsDuration: 2:25Kesi dhidi ya maafisa sita wa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS wanaotuhumiwa kwa kupotea kwa mvuvi Brian Odhiambo mjini Nakuru imeendelea leo ambapo mashahidi watatu walikuwa kizimbani. Watatu hao waliielezea mahakama jinsi walimuona Brian kwa mara ya mwisho akiwa mikononi wa maafisa hao. Kesi hiyo itaendela hapo kesho, ambapo shahidi mwingine mmoja atatoa ushahidi wake