Kesi ya utekaji nyara wa wanaume wawili yaanza

  • | Citizen TV
    1,824 views

    Chama cha mawakili nchini LSK kimemtaka Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja kufika mahakamani na kuelezea waliko Steven Kavingo na Kelvin Muthoni wanaodaiwa kutekwa nyara na maafisa wa usalama, Disemba mwaka jana. Katika kesi inayohusiana na kutekwa nyara kwao mawakili wanaowakilisha waathiriwa wanasema kuhakikisha usalama wa waathirwa inapaswa wakuu wa usalama kuwajibika. Kanja aliwasilishwa na wakili wake wakati wa kutajwa kwa kesi hiyo