Kituo cha saratani Kilifi

  • | Citizen TV
    152 views

    Serikali ya kaunti ya kilifi imepanga kuanzisha kituo cha Saratani kwa ushirikiano na Wakfu wa Agha Khan, Wakfu wa Bill and Melinda Gates na shirika la maendeleo la Ufaransa ili kuwashughulikia wagonjwa wa saratani nchini Kenya na Tanzania. Kaunti hiyo tayari imeingia katika Mkataba wa Maelewano na taasisi hizo huku huduma za kituo hicho zikilenga zaidi ya watu milioni Saba katika maeneo hayo. Mpango huo wa miaka minne pia utatoa ivifaa vya matibabu na mashine za uchunguzi wa saratani na programu za kupunguza vifo vya saratani.Hatua hiyo inalenga kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda sehemu za mbali kutafuta matibabu.