Chama cha walimu humu nchini KNUT kimelalamikia kuendelea kutekelezwa kwa sera ya uhamisho wa walimu licha ya ahadi ya serikali ya kuifutilia mbali. Chama hicho kinasema sera hiyo ni sawa na adhabu kwa walimu na inahatarisha umoja wa familia pamoja na afya ya akili ya walimu. Akizungumza mjini Kapsabet, kaunti ya Nandi, katibu mkuu wa chama cha KNUT, Collins Oyuu, aliitaka serikali kufutilia mbali sera hiyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive