Wabunge kutoka Magharibi wamtetea waziri wa afya Deborah Mulongo

  • | KBC Video
    41 views

    Kundi la wabunge kutoka eneo la Magharibi limemtetea waziri wa afya Deborah Mulongo dhidi ya kile walichotaja kuwa unyanyasaji kutoka kwa makundi ya wakiritimba na maafisa wa wizara ya afya. Wakiongozwa na mbunge wa Tongaren John Chikati, wabunge hao walidai waziri Deborah anahujumiwa na mmoja wa makatibu katika wizara ya afya ili aonekane kama mtu asiyefahamu majukumu yake. Wabunge hao wanaonya kuwa hawatakubali waziri Deborah kutishwa na kulaumiwa kwa changamoto zinazokabili mpango wa bima ya afya ya jamii, SHA.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News