Skip to main content
Skip to main content

Kundi la wakimbizi Nyanza ladai kubaguliwa

  • | KBC Video
    53 views
    Duration: 1:28
    Kundi la wakimbizi wa ndani kwa ndani waliopoteza makao wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008 linalilia haki kufuatia kile kinachotajwa kuwa ukosefu wa usawa katika kulipa fidia. Kundi hilo la eneo la Nyanza-Magharibi limewasilisha kesi kwenye mahakama kuu ya Kisumu likidai lilibaguliwa wakati wa mpango wa kuwapa wakimbizi makao uliopewa jina Rudi Nyumbani.Kupitia wakili, Moses Ombayo, kundi hilo linadai kwamba chini ya mpango wa Rudi Nyumbani, wakimbizi wa ndani kwa ndani kutoka maeneo ya Nyanza na Magharibi walipokea shilingi elfu kumi pekee kila mmoja ilhali wenzao kutoka maeneo mengine walidaiwa kukabidhiwa shilingi laki nne kila mmoja. Kesi hiyo iliyotajwa mbele ya jaji Joe Omido, itatajwa tena mwezi Januari mwakani. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News