Kuomboleza Injenda : Mudavadi aifariji familia

  • | KBC Video
    34 views

    Viongozi wa kisiasa wanaendelea kuomboleza kifo cha mbunge wa Malava Malulu Injendi, wakimtaja kuwa kiongozi aliyehubiri umoja na aliyejizatiti kufanikisha mipango ya kuunganisha taifa hili . Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, amemtaja Injendi kuwa kiongozi mkakamavu aliyejitolea kuanzisha miradi ya kuboresha maisha ya wakazi wa eneobunge lake Mudavadi aliyetembelea familia ya mwendazake kuwafariji katika mtaa wa South C,jijini Nairobi, pia alimuomboleza injendi kama mtu mwenye maono aliyedumisha heshima na taadhima . Injendi alifariki tarehe 17 mwezi huu na atazikwa juma lijalo nyumbani kwake katika kaunti ya Kakamega . Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive