KUPPET yataka polisi kuchunguza kupotea kwa mtoto Mombasa

  • | Citizen TV
    1,167 views

    Muungano wa walimu wa shule za sekondari na vyuo anwai (KUPPET) umetaka asasi za usalama kuharakisha uchunguzi kuhusiana na kutoweka kwa mtoto wa miaka mitatu aliyetoweka zaidi ya wiki mbili zilizopita. Kulingana na babake jeremiah nyamaseghe, ambaye ni mwalimu wa shule ya upili, kupotea kwa mwanawe kumesababisha majonzi kiasi cha kwamba hajaweza kwenda kazini kwa wiki moja sasa. Francis mtalaki anaunga nasi mubashara kutoka magongo mwisho kaunti ya mombasa.