Kwa nini uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi

  • | BBC Swahili
    284 views
    Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema uchumi wa nchi hiyo upo katika hali nzuri kwa sasa na kuna matarajio ya uchumi huo kuimarika zaidi baada ya kukumbwa na misukosuko ya kimataifa ikiwemo COVID-19 na vita vya Urusi na Ukraine. Hakikisho hilo limetolewa na Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba wakati wa mahojiano maalum na mwandishi mwandamizi wa BBC Florian Kaijage.