LSK yalaumu ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma

  • | K24 Video
    56 views

    Chama cha mawakili nchini, LSK, kimebaini kuwa ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa asasi mbalimbali za serikali ndio kikwazo kikubwa katika kupatikana kwa haki kwa wale waliouawa na kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kitaifa ya kizazi cha Gen Z. LSK pia imelaani ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (ODPP) kwa kudai kuwa inatatizwa na ukosefu wa mashahidi, ikilaumu afisi hiyo kwa kuwatamausha wananchi.