Maafisa wa KWS wadaiwa kumpiga risasi mkazi kijijini Kone, Tana River

  • | Citizen TV
    573 views

    Familia Moja kutoka Kijiji Cha Kone eneo bunge la Garsen Kaunti ya Tanariver inalilia haki baada ya jamaa yao kupigwa risasi na maafisa wanaodaiwa kuwa wa kitengo cha walinda Wanyama pori KWS mbele ya Familia yake. Inadaiwa marehemu Isack Jarso Delo mwenye umri wa miaka 50 alikuwa nyumbani kwake ambapo maafisa 20 wa kulinda Wanyama pori KWS walipomvamia. Hata hivyo, kwenye ripoti iliyotumwa kwa vyombo vya habari, idara ya KWS inasema kuwa mwathiriwa alikuwa na watu wengine walioshambulia maafisa wa kws kwa mishale yenye sumu kwenye mbuga ya wanyama, na hivyo akajeruhiwa na baadaye akafariki.