Maafisa wa Marekani na Ukraine wasema Kyiv inaunga mkono usitishaji vita...

  • | VOA Swahili
    30 views
    Maafisa wa Marekani na Ukraine wamekutana Jumanne mjini Jeddah, Saudi Arabia, kwa mazungumzo juu ya juhudi za kumaliza vita vya Russia na Ukraine, huku pande zote mbili zikisema Kyiv inaunga mkono pendekezo la Marekani la kusitisha vita kwa siku 30. Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mazungumzo hayo imesema, “Ukraine imeelezea utayari wa kukubali pendekezo la Marekani kupitisha mara moja sitisho la mud ala mapigano kwa siku 30. ambalo linaweza kuongezwa muda kwa makubaliano ya pande zote, na pia litasubiri Shirikisho la Russia kukubali na wakati huo huo kulitekeleza. Marekani itawasiliana na Russia na kuwa kukubali kwa Russia ndiyo msingi wa kufikia amani. - VOA #trump #zelenskyy #ukraine #russia #voa #saudiarabia #marekani