Maafisa wa serikali wanaoshirikiana na wanyakuzi wa ardhi waonywa

  • | KBC Video
    92 views

    Serikali imetangaza kwamba itakabiliana vilivyo na wanyakuzi wa ardhi wanaohusishwa na taharuki ya uskwota inayozidi kuongezeka katika kaunti ya Machakos. Akiongea baada ya kuongoza mikutano ya kampeni ya kudumisha usalama kwa jina Jukwaa la Usalama mjini Machakos, waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen alifichua kwamba maafisa wa ngazi ya juu serikalini,wanasiasa,maafisa wa polisi na wale wa ardhi pamoja na magenge ya wahalifu ni miongoni mwa watu wanaojishirikisha na biashara haramu ya ardhi, hali ambayo imeifanya kaunti ndogo ya Mavoko kuwa mafichoni makuu ya wahalifu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive