Maandamano ya kutaka Kizza Besigye aachiliwe Nairobi

  • | Citizen TV
    8,239 views

    Wanaharakati kutoka mashirika tofauti yasiyokuwa ya serikali, Chama cha Mawakili nchini na Muungano wa Madaktari wamefanya maandamano jijini Nairobi wakimtaka Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, kuachiliwa huru. Waandamanaji hao waliwasilisha malalamishi yao katika Bunge la Kitaifa kabla ya kuendelea na maandamano hadi katika ofisi za ubalozi wa Uganda nchini