Mabadiliko Serikalini I Makatibu wapya 14 wateuliwa

  • | KBC Video
    1,917 views

    Rais William Ruto amefanya mabadiliko katika nyadhifa za makatibu wa wizara ikiwemo kuwapandisha vyeo maafisa wakuu na kuwateua makatibu wapya. Miongoni mwa uteuzi huo ni Profesa Edward Kisiang'ani aliyeteuliwa kuwa mshauri mkuu na mwanachama wa baraza la rais la washauri wa kiuchumi ambapo mahala pake sasa pamechukuliwa na Stephen Isaboke, aliyekuwa afisa mkuu wa maswala ya udhibiti katika kampuni ya MultiChoice. Aliyekuwa waziri wa afya Susan Nakhumicha amepata jukumu jipya kuhudumu kama mwakilishi wa kudumu wa ujumbe wa kudumu wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu makazi, UN Habitat jijini Nairobi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive