Mabadiliko ya sera ya elimu yanatarajiwa kuwaandaa vijana katika soko la ajira

  • | VOA Swahili
    300 views
    Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, toleo la mwaka 2023, inalenga kutoa elimu na ujuzi kwa wanafunzi ili kuwaandaa kwa mahitaji ya sasa na ya baadaye katika soko la ajira na maisha kwa ujumla kupitia uhimizaji wa elimu ya ujuzi kuliko kutegemea taaluma pekee. Prof Carolyne Nondo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia amesema mabadiliko ya sera hiyo yanatarajiwa kuwaandaa vijana kushindana katika soko la ajira ndani na nje ya nchi pamoja na kuongeza kiwango cha elimu ya Tanzania kuwa shindani katika soko la ajira. #sera #elimu #tanzania #soko #ajira #wanafunzi #teknolojia #waalimu #diploma #voa #voaswahili