Mahakama yadinda kusitisha hoja ya kumtimua Gachagua

  • | Citizen TV
    4,900 views

    Mahakama kuu imedinda kwa mara nyingine tena kusitisha mchakato wa kumuondoa ofisini naibu rais rigathi gachagua. Jaji Bahati Mwamuye ameagiza kuwa kesi iliyowasilishwa na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha uda Cleopas Malala, iwasilishwe mbele ya jaji Chacha Mwita kwa maagizo zaidi. haya ni huku bunge likitaka masuala yote yanayohusiana na mchakato wa kumwondoa gachagua yajumuishwe kwani hoja hizo zinaibua masuala sawia. kesi 13 zimewasilishwa mahakamani kupinga kubanduliwa ofisini kwa Gachagua. Gachagua atapata fursa ya kujitetea bungeni hapo kesho.