Mahojiano na mwanaharakati Elisheba Eunice

  • | K24 Video
    14 views

    Kwa miaka mingi wanawake wameonekana kutengwa katika maswala ya umiliki wa mali haswa waume zao wanapoaga. Mfano ni dada huyu wa miaka ishirini na tano kutoka turkana ambaye wakati mume wake aliaga alinyang’anywa mali na kubaki na wanawe wawili.licha ya kwamba hili lingemfifisha, ilikuwa nafasi bora kwake Elisheba Eunice kuzinduka na kuanza safari ya kutoa hamasa kwa wanawake na wasichana kuhusu uwezo wao wa kumiliki ardhi. Haya ni kati ya yale ameyataja katika jukwaa la mwanamke na uongozi tulipokutana naye akiwa anahudhuria kongamano la ardhi ya jamii lililoandaliwa na shirika la impact kenya huko Samburu