Maimamu na viongozi wa kidini wapanga maandamano kupinga utekelezaji wa mtaala wa CBC

  • | Citizen TV
    1,045 views

    Maimamu na viongozi wa dini ya kiislamu ukanda wa kaskazini mwa Bonde la Ufa wamepanga maandamano kuanzIa tarehe 13 mwezi huu kupinga utekelezaji wa mtaala wa CBC. Viongozi hao wamesema mtaala huo ni ghali na unakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa miundo msingi.