Majangili washambulia watu kwenye barabara ya Marigat

  • | Citizen TV
    137 views

    Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wawili wakijeruhiwa katika shambulizi la majambazi lililotokea mapema asubuhi ya jana eneo la Loberer, kwenye barabara ya Marigat kuelekea Chemolingot. Waathiriwa, ambao walikuwa wakielekea katika soko la Nginyang, walivamiwa na majambazi wanaoshukiwa kuwa wamegeuka kuwa wanyang’anyi wa barabarani. Washambuliaji walilenga msafara wa wafanyabiashara uliokuwa ukisindikizwa na polisi, ambapo malori mawili yalishambuliwa kwa risasi. Hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo kutokana na mauaji ya wanaume wawili waliokuwa madereva, huku polisi zaidi wakipelekwa kuimarisha usalama. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika makafani ya Hospitali ya Kaunti ya Baringo.