Mamake Kibet: Nirudishieni wanangu!

  • | Citizen TV
    4,684 views

    Haya yalipokuwa yakiendelea, Mamake mchora vibonzo Gideon Kibet Bull na nduguye Ronny Kiplangat ambao pia nao walitekwa nyara sasa anasema anataka wanaowazuilia wanawe kuwarejesha. Mamake vijana hawa waliotoweka siku nne zilizopita amesimulia namna habari za kutekwa kwa wanawe zilivyomuathiri kiafya. Maryanne Nyambura alitembelea familia hii na hii hapa taarifa yake