Mamia ya waumini wafanya maombi kwenye Mlima Kenya

  • | Citizen TV
    9,690 views

    Mamia ya waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya walifurika katika mlima kenya kwa hafla ya maombi ya taifa huku wakilikemea visa vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka humu nchini haswa msimu huu wa krismasi. Akizungumza eneo la Samson Corner kwenye barabara kuu ya Mwea kuelekea Embu wakili Ndegwa Njiru ameitaka serikali ya kenya kwanza kuwapa wananchi ulinzi wa kutosha huku akimshutumu inspekta jenerali mkuu wa polisi Douglas Kanja akimtaka kuelezea wanachi nini haswa kinachoendelea nchini. Kulingana na waumini hawa,wananchi wanapitia hali ngumu ya maisha,huku wazazi ambao wanao wametekwa nyara na hawajulikani walipo, wakiendelea kuumia.