Mamlaka ya SHA yakosoa afisa mkuu wa TSC Nancy Macharia

  • | Citizen TV
    158 views

    Mamlaka ya Afya ya Jamii SHA imesistiza kwamba afisa mkuu mtendaji wa Tume ya Walimu Nancy Macharia aliipotosha Kamati ya Bunge kuhusu elimu kwa kudai kwamba SHA ilikosa kuwasajili walimu alfu mia tatu sitini katika mpango wa bima ya afya. Kwa Mujibu wa Usimamizi wa SHA Walimu wote wanaweza kusajiliwa katika mpango huo na wanaweza kufaidika kupitia huduma tofauti Kupitia taarifa SHA imedai kwamba ... Walimu wote na wana wao wanaweza kusajiliwa kwa Mamlaka ya Afya ya Jamii. TSC Inaruhusiwa kuwasajili walimu kwa mpango mwengine kwa manufaa zaidi . Huduma ambazo walimu wanaweza kufaidika nazo ni.. Mpango wa Afya ya msingi, Mpango wa Bima ya Afya ya Jamii na Mpango wa Dharura na magonjwa ya Muda Mrefu.