Wadau wa sekta ya elimu wamezitaka taasisi za elimu ya juu kushirikiana na wenye viwanda ili kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira la sasa.
Akizungumza wakati wa Wiki ya Maonyesho ya Fursa za Kazi katika Chuo Kikuu cha Zetech, bewa la Ruiru, Msimamizi wa kitengo cha Elimu katika chuo hicho, Profesa Owen Ngumi, alisema hatua hiyo itasaidia kukuza ubunifu na kufungua njia kwa vijana kupata ajira zenye heshima na fursa za ujasiriamali ndani na nje ya nchi.Wakati wa kongamano hilo, wanafunzi wa chuo hicho waliitaka serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kupanua wigo wa ajira.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News