Marekani, Japan na Korea Kaskazini wafanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja

  • | VOA Swahili
    498 views
    Wanajeshi wa Marekani, Japan, na Korea Kusini wamefanya mazoezi ya pamoja katika bahari ya kanda ya Asia Mashariki. Mazoezi hayo ni mapana na ya mwisho kabla ya rais Joe Biden kuondoka madarakani na kukabidhi uongozi kwa Donald Trump. Balozi wa Marekani nchini Japan Rahm Emmanuel amesema kwamba mazoezi hayo ya nchi tatu na ushirikiano wa kijeshi unatuma ujumbe mzito kwa Beijing. Kamanda wa wanajeshi wa Korea Kusini katika mazoezi hayo Hur Sung Jae, amesema mazoezi hayo ni ujumbe kwa Korea Kaskazini kwamba wapo tayari kujibu hatua yoyote ya uchokozi. Mazoezi yamefanyika baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu, mwezi uliopita. #wanajeshi #marekani #japan #koreakusini #joebiden #mazoezi #donaldtrump #koreakaskazini #beijing