Matabibu watishia kugoma mwezi huu

  • | KBC Video
    52 views

    Mgomo mwingine unanukia katika sekta ya afya, kufuatia makataa ya siku 14 yaliyotolewa kwa serikali na chama cha matabibu nchini (KUCO), kikitaja kuchelewa kutekelezwa kwa makubaliano ya kurejea kazini yaliyotiwa saini mwezi Septemba mwaka jana. Wakiongozwa na mwenyekiti wao wa kitaifa Peterson Wachira pia walishutumu halmashauri ya afya ya jamii (SHA) kwa madai ya ubaguzi. Walidai kuwa matabibu wamezuiwa kutoa huduma chini ya mfumo mpya wa bima ya afya, kutokana na bodi ya halmashauri ya afya ya jamii kushindwa kutambua vituo vya afya vilivyosajiliwa, na baraza la matibabu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive