- 4,931 viewsDuration: 3:16Seneta wa Nandi Samson Cherargei alijipata mashakani kutokana na matamshi yake ya kuunga mkono utekaji nyara wa wanaharakati wa kenya kwenye mataifa jirani. Cherargei aliyezungumza kanisani huko Kapsabet siku ya jumapili alipongeza viongozi wa Uganda na Tanzania kwa kukabiliana na wanaharakati na kusema kenya itamalizia pale walipowachia.Kanisa la KAG alikozungumzia Cherargei lilijitenga na matamshi hayo huku seneta huyo akishikilia kuwa hataomba msamaha.